Jean Claude Biharuhanga : Ukosefu wa usalama unazuia wagonjwa wa ukimwi kupata matibabu kwa mda muafaka

Tarehe moja Desemba kila mwaka, dunia inaadhimisha Siku ya kupambana na Virusi vya UKIMWI. Huko Bunia, Shirika lisilo la Kiserikali la Usambazaji wa Dawa za Kupunguza Ukimwi kwa Jamii, PODI, linasaidia karibu wagonjwa elfu moja mia ine kote jijini. Jean Claude Biharuhanga, mwenyewe anayeishi na Virusi vya UKIMWI, ni msaidizi wa utawala katika shirika hili. Anazungumzia hali ya wagonjwa wa ukimwi wanaoungwa mkono kupitia uhamasishaji na utunzaji wa kisaikolojia na kiroho. Jean Claude LOKY alimuhoji.

Source: Radio Okapi